Monday, June 6, 2011

Fisi ni fisi tu, kumbe mbunge ana mke kisu ile mbayaaaaa!


Huyu mama anaitwa Huma Abedin,ndio mama mjengo(mke) wa mbunge Anthony Weiner.Huyu mama sio tu kwamba ni msomi bali bata lake ni noomaaa,kwa taarifa yako huyu mama ni mmoja wa wasaidizi wa juu sana wa Hillary Clinton ambaye ni secretary of state huko mbelembele,hapa bibie Huma alikuwa akimfungulia mlango mama Clinton katika moja ya mavikao yao hukohuko washington ndo mapaparazi wakamfotoa,kwichaaaaaaaang!

Sijui haya ni mazingaumbwe au mazingaombwe?


Jamaa anaitwa Sufi Kalandar kutoka huko India akionyesha ufundi wa kuliengua jicho kutoka kwenye position yake,teh teh teh hapa ilikuwa ni kwenye sherehe moja ya kikabila huko kwao.Please Don't try this at home

Kama taa za disco vile?!


Hapa sio maisha club,billz ama stone club mwanza, club zinazosifika kuwa na lights za ukweli ndani....Hiki ni kimbembe cha volcano iliyoripuka huko kusini mwa nchi ya chile katika eneo la puyehuye siku ya jumamosi na kusababisha watu 600 wanaoishi kando ya eneo hilo kuwa-evacuated!

Happy birthday Philbert Kabago!


Mshkaji Phil leo ni birthday yake 6/06.Tatizo hatujui ametimiza miaka mingapi,sio issue.Mungu amzidishie miaka kibao kushinda hata ya mzee mandela wa kule sauzi!

NATO sio mchezo!!


Inawezekana Ghadafi ni kweli ana matatizo yake,lakini hii unayoitazama kwenye picha ndio hali halisi wanayoifanya Marekani na maswahiba zake wanaojiita MNATO oooops ni NATO kule Libya,sasa sijui wakitoka Tripoli watatua zao pale kati Dizim.U shud Ask yo self!

Duh, nilidhani wahanga wa gongo la mboto DSM!


Hawa ni watu wa kabila la Aborigines ambao naskia ndio wazawa halisi wa AUSTRALIA hukoooo uzunguni, lakini maisha yao ni duni balaa.Serikali inapenda kuwasaidia lakini inalalamika kwa kabila hilo kutopenda kujishughulisha.Viongozi wa kabila hilo pia wanailalamikia serikali kwamba haiwajali.Hii inaitwa nani amfunge paka kengele!!!

Ruff rydeeeeeers first lady


Unazikumbuka Gangsta lovin,Love is blind,Blow your mind n.k?Anaitwa EVE kutoka ruff ryders ya kina DMX aliyetesa miaka kadhaa iliyopita.But kwa sasa mwanadashosti huyu she's thinking about gettin married an havin kids mh mh,Utu uzima hauibishi hodi una-penetrate kutokana na maamuzi tu.Cheki anavyosema ye mwenyewe-"I want marriage, I want babies, soon, but later. I'm seeing someone at the moment. I'm not saying [who it is], but it's been a year. It's not a secret. He's not a music celebrity." Kwa taarifa yako njemba yake inaitwa Maximillion cooper, anaendesha vile vigari vya mashindano!