Wednesday, June 8, 2011

MITI MINGINE BWANA!!


Jamaa ni kama anajiuliza".hivi huu mti unaitwaje."

WAPI KUFULI FAZA MBONA ZE @#$%$#@ INANING'INIA!?


Watoto siku zote wana maisha ya tofauti sana.Waacheni waje kwangu maana ufalme wao ni wa mtu kama mimi!

DOLE LA KATI, NOMA KWAKO!


Mtoto kama huyu akikua akiwa kama Eminem hatuwezi kushangaa,sasa hilo dole la kati anamwonyesha nani kama sio laana kum!

SAIDIA BABA!!!


Matonya's all around,hata wanyama wanajaribu kuangalia utaratibu wa kupata msaada yakinifu!

SIAFU NOMA SANA,HAWAJUI NIKO MBELE ZA WATU?


Dah sista duu imekuwa ngumu kuvumilia wadudu waliokuwa wanauma sehemu nyeti a.k.a ikulu.Akaona sio issue,ngoja asaule viwalo acheki mzigoni kunani tena???

MTOTO ZIWA,CHUCHU SAA SITA!!


Mwana wa malkia wa uingereza Prince Charles hapa anaonekana kama anataka kumshika nyonyo huyo dada mwanajeshi,shosti naye anacheeeeka dah,kazi kweli kweli.Kila mtu na mtuwe bwana!

WATOTO WANAMIDOMO MIKUBWA LAKINI SIO KAMA HUYU!


Hakuna kitu kinachokera kama sisi tunaokaa nyumba za kupanga, hazina cieling board halafu chumba cha jirani kuna mtoto anakuwa analia hasa mida ya usiku ambapo tunataka kujipumzisha.Sipati picha mtoto kama huyu atapiga kelele kiasi gani pindi atakapoamua kufungua mdomo wake kwa kilio!

GET ME TO THE AIR PORT and DON'T SPARE THE HORSES!!


Inapofikia kwamba tunahitaji usafiri kwa hali na mali hatuna budi kuwa wabunifu kama mshkaji wetu hapa,yeah safi sanaa!

Mr bean kumbe ana mtoto?


Mr bean huenda ndio mchekeshaji wa karne,watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu familia yake,here i'm trying to convince you kwamba huyu katika picha ni first born wake,would u believe it?!

THUG LOVING!

Rapa ja rule hatimaye amejisalimisha mwenyewe mahakamani huko manhattan na ataanza rasmi kutumikia kifungo cha miaka miwili jela akikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na silaha aina ya bastola. Kabla hajaingia kortini ja alionekana akisaini autographs za mashabiki wake nje ya mahakama huku akiwaaga"see you in 18," akaongeza na neno"one love",akapigwa pingu huku akiiangalia familia yake akiwemo mama yake,mke wake aitwaye Aisha ambao wote walikuwa wakilia kwa huzuni,kwa pamoja wakamwambia"LOVE YOU".Bongoshega inasema"tutakukumbuka ja rule coz ulikuja bongo na ukatupa burudani ya ukweli".WE'LL BE MISSING U NEGRO!

BAKA BOYZ!


Wakali wa michano from Rock city mwanza,wanaitwa BAKA BOYZ ambao wanasikika na ngoma zao za ukweli kama vile Huu ndo muda,kichurachura pamoja na naongea na vijana.Hapa walikuwa wamemaliza kufanya interview katika kipindi cha michano time ya Passion Fm mwanza siku ya wednesday 8/06/11.from left to right ni Biznea,Roland na Kadgo.Washkaji hawa wanapatikana maeneo ya nyakato,mecco south, Rock city,ukitaka kuwasikiliza vema wee tune tu Passion fm utawagumia live.Tunasubiri mzigo wa album hopin ita-drop very soooon!

MANCHESTER UTD NA USAJILI!


Katika harakati za kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao tayari babu alex ferguson wa manchester united amefanikiwa kumnasa beki Phil jones kutoka blackburn rovers ya hukohuko uingereza.

KICHWA KIMEOTA KICHWA!


Bondia HASIM RAHMAN akiwa na nundu saizi ya mpira wa baseball.Hii ilikuwa ni katika pambano la uzito wa juu kati yake na EVANDER HOLYFIELD,JUNE, 2003,pambano hilo lilimalizika kunako raundi ya nane kutokana na RAHMAN kuwa na majeraha mabaya usoni na holyfield akapewa ushindi.Baada ya pambano rahman akahojiwa na akongea maneno haya ya kidhungu-"I DIDN'T THINK HE COULD DO SO MUCH DAMAGE WITH HIS HEAD. HE MUST HAVE A METAL PLATE IN THERE OR SOMETHING...I HAVE A CUT IN THE MIDDLE OF MY FOREHEAD, AND AN EXTRA HEAD ON MY HEAD."

Heh,huyu ni handsome au hendisamu?


Kwa style ya nywele za huyu kijana naingiwa na imani kuwa binadamu wa mwanzoni enzi za zama za kale za mawe walikuwa ni masokwe!

DRUNK & SMOKING CAT!


Mr nyau akiwa nduki kinoma baada ya kufakamia pombe, mdomoni kaweka fegi halafu kazimika.Kakosa kibao tu pembeni ambacho kingeandikwa DO NOT DISTURB

Pwaaaaaaah!


Huyu bonge alijirusha kutoka gorofa ya juu sana,alipofika chini ndio akawa kama unavyomcheki hapo!

Jos Mtambo!

!

Jose Mtambo wa kigambo, mmoja kati ya washkaji wa bongo wanaokaza katika hip hop ile kinoma noma,hivi karibuni amedondosha dude moja hivi linaitwa BATA BOY akiwashirikisha masela wengine kibwena kama vile Babuu wa kitaa,cowboy ngwea,Fid Q The don Ngosha na baba jonii Adam Mchomvu.Hilo dude baya sana unaweza ukawa unalisikiliza kupita Passion fm ukiwa dar,Arusha ama rock city mwanza,sana tuuuu!